Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Majibu ya haraka kuhusu ibada, uanachama, sadaka na mahali tulipo.
Ibada za Jumapili zinaanza saa ngapi?
Ibada kuu huanza saa 2:00 asubuhi (08:00). Ratiba kamili iko kwenye ukurasa wa Mwanzo.
Kanisa liko wapi?
Makao makuu yako Mbezi Louis, barabara ya Goba, nyuma ya Shule ya Msingi Louis na mkabala na Kanisa Katoliki. Tawi lingine liko Kibamba, Ubungo.
Nitajiungaje na kanisa?
Jaza fomu ya uanachama (mtandaoni au kanisani). Mchungaji atawasiliana nawe, kisha utahudhuria darasa la waumini wapya.
Ninawezaje kutoa sadaka nikiwa mbali?
Tumia M-Pesa, Mixx by Yas (Tigo Pesa), Airtel Money au benki. Maelekezo ya hatua kwa hatua yako kwenye ukurasa wa Toa Sadaka.
Je, kanisa limesajiliwa?
Ndiyo. CFC (T) imesajiliwa kama Bodi ya Wadhamini; katiba ilipokelewa na RITA, Dar es Salaam, tarehe 11 Machi 2021.
Naweza kuomba maombi au ushauri wa kichungaji?
Ndiyo. Tumia fomu ya Mawasiliano na uchague "Ombi la maombi" au "Ushauri wa kichungaji", au piga +255 656 552 392.